Sherehe ya Kupaa Bwana
Mt 28: 16-20
Sote tuna
tabia ya kushikilia tunachokifahamu na kukiamini. Tunaweza hata kupinga
mabadiliko ambyo yanaweza kuhatarisha maslahi yetu. Tunajiamini katika kuchagua
au kutekeleza tunachokijua vizuri. Kwa mafano, mtu hawezi kujiamini kutumia
barabara ambayo hajawahi kutumia kwend mahali anapokwenda hata ikiwa barabara
anayoifahamu ni ndefu na yakuchosha. Hata hivyo maandiko, yanatuhamazisha
kupambana na woga wa mabadiliko na vitu vipya ili tugundue kusudi la Mungu na
upendo wake kwetu. Tukijua tutavuka mipaka tuliyojiwekea kama Abraham na Sara,
Ruthu na naomi, Marimu na Yosefu na wanafunzi wa Yesu ambao walithubutu kushika
maono kubwa ambayo Mungu alikuw nayo kwa ajili yao. Wote walishi maisha mapya
ambayo awali hawakufahamu. Sikukuu ya kupaa kwa Yesu tunayosherekea inatupa
hamasa ya kuwa na ujasiri wa kuacha mazoea na kukubali hali mpya baadaye.
Wanafuni walitaka
kumkariri Yesu wa kwama kabla hajafa na kufufuka, walisita kumruhusu aende
zake. Lakini walipata changamoto ya kuanza uanafuni uliokuwa umeanzishwa na
Yesu. Utengano wa Yesu na wanafunzi wake unaleta nmna mpya ya uwepo wake na
hatimaye kuanza maisha mapya. Kupaa kwa Yesu hakukuwa kutoweka kwa Yesu. Badala
yake ni mwanzo na namna upya ya uwepo wake. Yesu hakutawaliwa tena na sharia za
mahali wala wakati. Kwa kupaa, anauwezo wa kuwa na wanafunzi wake wakati wote,
mahali popote. Wakati wa huduma yake ya kidunia angeweza kuw sehemu moja kwa
wakati mmoja. Ikiwa angekuwa huko Yerusalemu asingekuwako kapernaumu; ikiwa
angekuwa huko kapernaumu asingekuwako Yerusalemu. Lakini sasa kwa kuwa
ameunganishwa na Mungu, yuko popote alipo Mungu; na hiyo ni kila mahali.
Kuondoka
kimwili kwa Yesu kunafungua sura mpya katika maisha yao na maisha ya Kanisa. Sikukuu
ya kupaa ni kusherehekea mstakabali wa kanisa wake. Je! Tuanweza kujifunza nini
kutokana na sikukuu ya leo?
1. Sherehe ya leo inatualika kuiishi Imani yetu na
kujitoa kwa ajili ya Bwana. Kama Yesu alitegemea wanafunzi wake katika utume
wake, kwa sasa anatutegemea sisi. Utume wa Yesu haukuwa kwa wachache tu, lakini
kwa waumini wote. Sisi sote tumepewa jukuma la kwenda kutangaza Inili ya uhai
na upendo, tumaini na Amani, kwa ushuhuda wa maisha yetu. Tunahitaji kuwa
watangazaji na waenezaji wa injili; wote waliobatizwa, bila kujali nafasi zao
kanisani, ni mawakala wa uiinjilisaji.
2. Sherehe ya leo inatupa uhakikisho kuwa Yesu angali yupo, yupo hata wakati wa
uchungu na huzuni tunaopitia. Kwa kupaa kwake, Kristo hajatuacha lakini
amewezeshe Roho Mtakatifu kuingia katika maisha yetu. Kwa njia hii inawezekana
kwa kila mmoja wetu kubadilishwa na nguvu ya Roho Mtakatifu kuwa wakala au
chombo cah Kristo.
3. Yesu
alitufundisha masoma ya Imani, Matumaini, msamaha, rehema, ukombozi na upendo. Hatuwezi
kuweka masomo haya kwenye shelufu na kuyapuuza. Yanasimama mbele yetu katika
utu wa Yesu. Ingawa hayupo tena katika ulimwenguni wa mwili, lakini anaishi katika
neno lake. Lazima tufanye neno lake kuwa halisi katika maisha yetu na katika
maisha yaw engine. Ukristo ulikusudiwa kuwa Imani ambayo wafuasu wa Yesu
wangesaidia na kuwajali wengine, kama vile Yesu alivyokuwa anafanya, na kwa
kufanya hivyo watamjali Yesu ndani yao.
Nawatakia Jumapili njema.
No comments:
Post a Comment