Saturday, June 20, 2020

Jumapili ya 12 ya kawaida
Injili. Mt. 10:26-33


Injili ya leo ni mwendelezo wa maagizo ambayo Yesu aliwapatia mitume kumi na wawili alipokuwa anawatuma kwenda kutangaza Habari Njema za Ufalme wa Mungu. Maadili ya Ufalme wa Mungu ni tofauti na maadili ya ulimwengu; kwa hivyo watu hawapendi ujumbe wa wanachukia mitume. Kwa hivyo ilikuwa kawaida kwa mitume kuogopa wakati Yesu anawatuma kwenda kueneza injili kwa ulimwengu wenye uhasama. Labda, Yesu alikuwa amegundua kwamba wanafunzi wake wangeacha utume wao ili kuokoa maisha yao dhidi ya watu waliowachukia. Ndiyo maana Yesu aliwaambia wasiogope. Katika Injili ya leo Yesu anatoa sababu tatu kwa nini mitume wake, hawapaswi kuogopa kama asemavyo, 1.Mungu hakubali uovu kushinda wema, 2. Ni Mungu tu anayeweza kuua roho na mwili, 3. Mungu ni mwenye huruma na rehema. Wacha tautafakari yaya, moja baada ya jingine.
Yesu Kristo anabaini aina mbili za uoga ambao mitume walikuwa nao: kuogopa mashtaka ya uwongo na kutuhumiwa, na hofu ya kifo. Yesu mwenyewe alishtumiwa kwa uwongo mara nyingi na watu wake mwenyewe na viongozi wa kirumi, walileta mashahidi wa uwongo dhidi yake, ilia ache utume wake, ili kumtenganisha na watu. Lakini Yesu hakuwahi kuogopa viongozi, badala yake aliutangaza Ufalme wa Mungu duniani. Kwa kuwa Yesu mwenyewe alikuwa amepata mashtaka ya uwongo na kukataliwa na watu, alijua kuwa hata wanafunzi wake watapitia hali hiyohiyo. Kwa hivyo Yesu aliwahimiza wanafunzi wake wasiogope mashtaka ya uwongo wala kutuhumiwa. Na anawahakikishia kuwa Mungu atafichua mipango mibaya na vitendo vya watawala kwa kusema; "Hakuna kitu kilichofichwa ambacho hakitafichaliwa" Kwamba “Mungu hatakubali uovu kushinda ni ahadi ya suya ya 26. Yesu anawahakikishia wanafunzi wake uhakika na uthibitisho wa Mungu.
Pili, wanafunzi pia waliogopa kifo. Sote tunaogopa kifo. Tishio la kifo linaweza kuwa lina nguvu Zaidi ya hofu ya kushitakiwa. Kwa kutangaza neno la Mungu, inawezekana kwamba wanafunzi waliuawa. Tumeshuhudia katika utamaduni wetu wa KiKatoliki kwamba, karibu mitume wote waliuawa. Wengine wao walisulubiwa msalabani, kama Peter na Andrea, na wengine kama Yakobo, Paul, na Bartholomeo waliuawa kikatili. Serikali katika nchi nyingi hutumia hofu ya kifo dhidi ya Wakristo. Yesu anakiri kwamba wanadamu wana nguvu ya kuua, lakini anabainisha kuwa wana nguvu tu ya kuua mwili, sio roho. Ni Mungu pekee anayeweza kuua roho na mwili. Kwa hivyo, Mungu pekee ndiye tunayepaswa kumwogopa.
Sababu ya tatu kwa nini wanafunzi hawapaswi kuogopa ni upendo na huruma ya Mungu. Sisi ni muhimu sana kwa Mungu kuliko shomoro. Mungu anajua kila kitu tunachopitia. Yesu hkuahidi maisha rahisi kwa wafuasi wake. Yeye aliwaeleza wazi changamoto na mapambano ambayo wangekutana yao lakini aliwahakikishia kuwa Mungu hujali Shomoro ambazo zinauzwa, kwa hiyo anawajali Zaidi wanafunzi wake kuliko shomoro. Mngu anatujua, anatujali ndiyo maana anafahamu hata idadi ya nywele zilizopo vichwani mwetu.
Je! Tunaweza kujifunza nini katika Injili ya leo? Usomaji wa maandiko ya leo unatutaka tusiogope, unatualika kuwa mitume wa Kristo, kuwa thabiti katika Imani yetu na kuwa wafuasi wa Yesu na washiriki wa Kanisa bila woga. Maisha yetu na witi wetu ni tofauti na wito wa wanafunzi wa kwanza. Hofu zetu znatofautiana na Wakristo wa kwanza. Kuna mambo mengi ambayo tunaogopa. Wakati mwingine tunaogopa kwamba tutafanya uamuzi mbaya. Wakati mwingine, tunaogopa kama wengine watakavyotufikiria tukimtangaza Yesu. Tunaogopa kwa kuwa hatujui hatima ya watoto wetu baadaye. Tunaogopa pia uzee. Wakati mwingine tuanaogopa pia kitakachotokea ikiwa tutaugua. Mzizi wa hofo hizi ni woga wa kupoteza na kukosea. Kila hofu tuliyonayo imewekewa msingi kwa kujua kuwa tuna kitu au mtu wa kupoteza. Ninaweza kupoteza kazi yangu, familia, nyumba, pesa, afya na hata maisha yenyewe. Kukataliwa na kupoteza ni msingi wa hofu yetu. Lakini tunasahau jambo moja; Magumu, shida na matitizo yanayotukabili, Mungu wetu anayajua kuliko sisi tunavyoyajua. Baba yetu wa mbinguni anajua kabisa kile kinachotokea. Tukishajua tu ya kwamba Mungu yuko upande wetu na maisha yetu yamo mikononi mwa Mungu atupendaye, tunaweza kuishinda hofu. Wakati mwingine hofu ikituvamia tunapaswa kukumbuka kuwa tunaye Yesu, kuwa waaminifu kwa Yesu tukimtumainia Yesu katika maisha yetu, yeye ana nguvu kuliko uoga na hofu zituzongazo. Nikukumbushe kuwa Mungu anatujali- sisi ni watoto wake wapendwa, na anamjali kila mmoja wetu. “Usiogope; wewe ni wa thamani Zaidi kuliko shomoro wengi.” Mstari wa mwisho wa zaburi 27 unaelezea kwa muhtasari: “Mtumaini Bwana. Kuwa na Imani; usikate tamaa. Mtumaini Bwana.”

Siku moja padre moja alikuwa maekaza kuhubiri kwa bidi sana katika mkutano, kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu, na hawakupaswa kuogopa wakati hali mbaya inapofika. Watu walufurahiswa sana nah ii na wote walishangilia wakisema amen. Ghafla gaidi akaingia kanisana na bunduki. Na akaelekezea bunduko kwenye mkutano akisema, “ Ni nani mtoto wa Mungu hapa? Nataka nimpeleke mbinguni? Mkutano ulikaa kimya. Kisha akafyatua bunduki na kupiga paa, mkutano ukapiga kelele, “Ni Padre, Yeye ndiye anasema kila wakati kuwa yeye ni mtoto wa Mungu! Padre akajibu ni njama ya aina gani hii? Kila mtu hapa anajua kuwa mimi ni mtoto wa Charles Githinji.

No comments:

Post a Comment

Sermon for 17th Sunday in Ordinary time, Year A.

Sermon for 17th Sunday Ordinary time, year A. Gospel. Mt. 13: 44-52 In the Gospel of today, we are presented with three ...