Somo la Kwanza. Kut. 34: 4b-6, 8-9
Somo la Pili. 2 kor. 13:11-14
Injili. Yn 3: 16-18
Je, tunaelewa nini kuhusu utatu Mtakatifu wa Mungu?
Zamani za kale katika kijiji kimoja nchini Nigeria mzungu mmishionari alifika
na kwanza kufundisha wenyeji kuhusu Ukristu. Kwanza alitaka kuanza kufundisha
kuhusu utatu Mtakatifu. Alianza kwa kusema ya kwamba kuna Mungu mmoja tu. Halafu
akafundisha kuwa kuna mwana wa Mungu na jina lake ni Yesu. Mzee mmoja akamuliza
mmishionari, ulituambia ya kwamba kuna Mungu mmoja tu, na sasa unaongea kuhusu
mwana wake. Hii inamaanisha Mungu ana mke basi. Watu wakamuunga mkono mzee yule.
Mmishionari akajibu, sijasema kuwa Mungu ana mke. Makalio yako ndiyo yamesema
kuwa Mungu alikuwa na Mwana, kwa hiyo kama alikuwa na mwana ni lazima alikuwa
na mkee pia. Akasema huyo mzee. Mmishionari akampuuza mzee yule na kuendelea na
mafundisho yake kuhusu utatu Mtakatifu. Mwishowe yule mzee akamuona mmishionari
kuwa ni mwendawazimu. Alimpuuzia yule mmishionari na kuamua kwenda kunywa pombe
ya mnazi. Deturi ya kikristo inamwonesha Mungu katika utatu; Baba, Mwana na
Roho Mtakatifu. Utatu huu ni Mgumu sana kuelezea kwa wakristo.
Katika mafundisho ya katekisimu tunaulizwa kila mara,
Mungu ana nafsi ngapi? Huwa tunajibu kwamba, kuna Mungu Babu, Mungu Mwana na
Mungu Roho Mtakatifu. Na katekista akituuliza, Je? Kuna Mungu watatu? Tunajibu-La,
kuna nafsi tatu katika Munug Mmoja. Tunaporudi jibu namna hii tunapandishwa
viwango na kuwa waumini wa kanisa. Ni sawa na kusema moja kuongeza moja, na
kuongeza moja ni sawa na moja. Fundisho la Kiroho siyo somo la hesabu. Tunapaswa
kujiuuliza mafundisho kuhusu utatu Mtakatifu yanatuambia nini juu ya uhusiano
wetu na Mungu? Tunaelewa nii juu ya uhusiano huu? Kuna maandiko mengi na ishara
katika agano jipya ambayo yanaongea juu ya Utatu Mtakatifu. Maandiko haya na
kanuni hizi zilitumiwa na mababu zetu wa Imani katika desturi Fulani. Lakini kuna
maswali ya kutafakari katika mazingira yetu ya kiafrika. Kama mtanzania,
ninelewa nini juu ya Utatu Mtakatifu wa Mungu? Kuna chochote katika misingi ya
kiafrika kinachoweza kutuonehsa na kutufundisha kuhusu Utatu Mtakatifu wa
Mungu. Kuna viashiria mbalimbali vinavyoweza kutudhihirishia utatu Mtakatifu wa
Mungu. Pia ni Muhimu kutambua hizo ishara. La shivyo tutabakia kama huyo mzee
wa Nigeria hatuwezi kuuelewa Utatu Mtakatifu wa Mungu.
Katika vijiji vyetu, ninauhakika umewahi kumwona
mwanamke aliyebeba chungu kichwani mwake na mtoto amefungwa mgongoni akielekea
nyumbani kutayarisha chakula kwa familia yake na labda ni mjamzito. Taswira hii
ya mama wa kiafrika inatupatia njia ya kuelewa kuhusu Utatu Mtakatifu. Picha ya
mama anayebeba maji, mtoto mgongoni n mwingine tumboni inatupatia picha ya
Mungu anayejengwa sehemu nyingi, nafsi nyingi, uhalisia mwingi, na ubora mwingi
kwa wakati umoja akiwa Mungu Mmoja. Mungu wetu kama mama wa kiafrika anaunganisha
sehemu nyingi mungu wetu ni Mungu Mama, Mungu Baba, Mungu mwana, binti,
kaka, dada na wakati huo huo ni Mungu yule yule. Hii ndiyo njia rahisi mojawapo
tunayoweza kuitumia kueleza juu ya Mungu wa Utatu katika desturi za kiafrika.
Utatu Mtakatifu ni kama ishara kwetu tumekombolewa na Mungu kupitia Yesu Kristo, mwana wake
wa pekee kwetu kwa kufa na kufufuka kwake. Tunakumbushwa kwamba tunaokolewa na
Mungu kupitia kwa Yesu Kristu katika nguvu za Roho Mtkatifu. Kwetu sisi wa
Kristu Utatu Mtakatifu ni njia yetu ya pekee kumweleza Mungu na kile
alichotufanyia na anachoendelea kutufanya katika maisha yetu. Mungu anafunuliwa
kwetu kwa njia ya Kristu na ndani ya Kristu. Tunajua Mungu kama Baba, Mwana na
Roho kwa sababu Yesu alikuja kutuokoa kwa msaada wa Roho Mtakatifu na
anatuonyesha njia ya kuelekea kwa Mungu.
Hivyo katika sikukuu ya leo tunajifunza nini? Tunakumbushwa
kuomba ishara ya msalaba tukiwa na maana na heshima kubw. Inaunganisha fumbo la
utatu Mtakatifu na ishara ya ukombozi wetu kwa kuteswa kwa Yesu, kifo na
ufufuko wa Yesu. Tufanye ishara ya msalaba kwa heshima na hadhi kuu na kwa myo wa
sala ya kweli. Tunahitaji kuona utatu kama mfano mwema kwa familia zetu za
Kikristu. Tumeumbwa kwa upendo tuwe jumuia ya watu wenye upendo, kama vile
Baba, Mwana na Roho wameungana katika upendo. Umoja na furaha katika uhusiano
wa Baba, Mwana, na Roho ndiyo mfano mwema kwetu katika uhusiano wa familia za
wakristu. Familia zetu zinakuwa za Kikristu tunapoishi katika uhusiano wa
upendo na Mungu na watu wengine.
Tunaalikwa tuwe bora kama Mungu wa Utatu Mtakatifu
katika uhusiano wetu wote. Jamii za
kisasa wanafuata mtindo wa mimi ni mimi, wa kibinafsi. Lakini mafundisho ya
Utatu Mtakatifu uatupatia hamasa ya kuiga mtindo wa umoja, “Mimi na Mungu na
Jirani.” Nitakuwa mkristo iwapo ninafuata upendo wa Mungu kwa watu wote. Kama wana
wa Mungu tunaalikwa kujenga maisha ya upendo katika familia zetu, kanisa,
jumuiya na nchi. Kama Mungu mwana tunaalikwa kuwa wapatanishi, kutengeneza Amani.
Kama Mungu, katika Roho Mtakatifu ni jukumu letu kujifunua na kufundisha kweli
ili kuondoa giza la kiroho. Utatu Mtakatifu atuletee upendo, Amani na umoja
katika Roho zetu, familia, kanisa na katika nchi yetu ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment