Mt. 13: 24-43
Nilipokuwa
mdogo, mara nyingi mama yangu aliniambia kuwa, kama nitafanya kazi kwa ustadi,
kwa bidi na ni kawa mwema kwa kila mtu; kila nikitakacho maishani mwangu
kitafanikiwa. Ninaamini hivyo ndivyo wengi wetu tunaamini. Watumwa kwenye mfano
wa leo hawana tofauti na sisi. Katika injili ya leo, watumwa walijua kwamba
walipanda mbegu nzuri kwenye mashamba yao. Lakini walishangaa walipoona magugu
shambani. Walitaka kujua nini kilitokea na ni nani aliyepanda magugu shambani.
Bwana akasema, “adui ndiye kupanda.” Hasemi Zaidi. Yeye hajamtaja adui. Hakuwaamuru
wafanyakazi wake kumtafuta, na kumwadhibu adui. Watumwa walimwuliza bwana,
magugu haya yametoka wapi? Je! Tuyafanyeje? “Je! Tuyang’oe haya magugu? Bwana
akajibu, hapana, kwa maana mnapong’oa magugu mnaweza kuyang’oa pamoja na ngano.
Je! Kwa nini
mmiliki wa shamba aliwazuia kuyang’oa magugu? Tunaweza kufikiria sababu mbili. Kwanza,
bwana alijua kwamba ngano itapona licha ya uwepo wa magugu. Magugu yanaweza
kuvuruga ngano hiyo kwa muda tu lakini hayataharibu kabisa nganoau kuva shamba.
Pili, alijua jinsi ilivyo ngumu kutofautisha kati ya ngano na magugu. Vilionekana
kufanana. Vina rangi sawa, ukubwa sawa na majani yanaonekana kufanana nay a ngano.
Mtu anaweza kuvichanganya. Ni wakati wa mavuno tu unapoweza kuvitafautisha kwa
matunda yake. Nikiwaagiza ingekuwa inawezekana kuyatofautisha vizuri magugu na
ngano, Bwana asingewazuia. Lakini aliwazuia kwa sababu moja, msije mkakusanya
magugu, na kuzing’oa ngano pamoja nayo.”
Yesu
alitumia hadithi ii ya magugu na ngano kwa watu. Ukweli, kulingana na Yesu, ni
kwamba maisha yetu na ulimwengu wetu ni uwanja ambao mtu mzuri na mbaya
wanaishi, maisha na kifo vinakaa, shangwe na huzuni viko pamoja, kile
tunachotaka na kile ambcho hatutaki hukua na kuishi pamoja. Ngano na magugu
hukaa pamoja katika ulimwengu wetu na katika maisha ya kila mmoja wetu. Yesu anataka
waovu wasiondolewe akitumaini siku moja watatubu na kuwa ngano. Yesu anataka
kutoonyesha kuwa njia za Mugnu si njia zetu. Anatuambia, “ndio jinsi Mungu
anavyowavumilia watenda dhambi.”
Kumbuka, “mwizi
mwenye hekima ambaye alisulibiwa pamoja na Yesu? Je, anaweza kufananishiwa na
ngano au magugu? Labda tungekuwa tumekisia kwamba yeye alikuwa gugu kubwa, gugu
baya na tungekuwa tumekosea. Saa ya mwisho akawa ngano. Je! Tungemfikiria kama
angekuwa gugu wakati alipopata utawala? Wanafunzi ambao Yesu anaongea nao mfano
huu ni pamoja na Yuda ambaye baadae alimsaliti, Petro, ambaye baadaye alimkana,
Tomasi, ambaye baadae alimtilia wasiwasi
na Yakobo na Yohane, ambao wanathamini mambo yao kaibinafsi. Mwishowe, ni Yuda
pekee aliyepotea , akituonyesha kwamba “magugu” mengi yanaweza kuwa mavuno
mazuri mwishoni.
Je!
Tunaweza kujifunza nini katika kwa Injili ya leo? Kila mmoja wetu ni
mchanganyiko wa ngano na magugu. Yesu anaonyesha kupendezwa Zaidi na ukuzaji
kuliko kuondoa. Yuko tayari kungojea na kuwa na kuvumilia. Ikiwa sisi ni
wafuasi wake sis pia tuyavumilie magugu yaliyotuzunguka katika maisha yetu. Tunahitaji
kufanya mazoezi ya kuvumiliana sisi kwa sisi. Imani yetu katika Yesu Kristo
inatufundisha kuwa kila kitu kinachotokea katika maisha yetu, iwe; furaha, Baraka,
machungu na huzuni vinatokea kwa sababu. Kwa hivyo kama wafuasi wa Yesu Kristo
lazima tuwe na uvumilivu.
Miaka mingi
iliyopita, kulikuwa Mfalme moja. Mfalme alikuwa na mtumwa wa kiume ambaye,
katika kila hali alimtia moyo mfalme akisema, “Mfalme wangu, usikate tamaa, na
uwe na subira kwa sababu kila kinachotokea katika maisha yetu, kinatokea kwa
sababu.” Siku moja walienda kuwinda, wakati wanawinda mnyama pori,
akamshambulia mfalme, mtumwa huyo aliweza kumuua mnyama huyo lakini mfalme huyo
alipoteza kidole kimoja. Basi mfalme akasema; kama Mungu angekuwa mwema,
nisingeshambuliwa na kupoteza kidole hata kimoja. Mtumwa akajibu, “kila
kinachotokea katika maisha yetu kinatokea kwa sababu, kuwa mvumilivu, Mfalme
hakufurahiswa na jibu la mtumwa wake hivyo akamkamata mtumwa wake. Alipokuwa akienda
gerezani, alimwambia mfalme tena, kila tu kinatokea kwa kusudi, Mungu ni mwema
na mzuri. Siku nyingine, mfalme alienda kuwinda tena akiwa peke yake, siku hiyo
alitekwa na watu wanaotoa watu kafara. Hao watoa kafara walipokuwa madhabahuni,
waligundua kwamba mfalme hakuwa na kidole kimoja walimwachia kwa sababu
walimwona “ana kasoro” kutolewa kwa miungu. Aliporudi kwake ikuli, aliamuru
kuachiliwa kwa mtumwa wake akasema; rafiki yangu, Mungu amekuwa mzuri sana
kwangu. Karibu niuawe lakini kwa kukosa kidole kimoja, nimeponyoka kuuawa. Lakini
nina swali; ikikwa Mungu ni mwema, ikiwa kila kitu kinatokea kwa kusudi, kwa
nini anliniruhusu nikuweke gerezani? Mtumwa wake akajibu; Mfalme wangu, kama
nisingekuwa gerezani, ningeenda pamoja nawe, na ningekuwe nimeuawa na kutolewa
kafara, kwa sababu nini vidole vyote. Kila wakati Mungi ni mwema, yeye huwa
hana makossa, chochote kinachotokea katika maisha yetu, hufanyika kwa kusudi. Mungi
ni mwaminifu sike zote, na tunahitaji tu kumtegemea.
Injili ya
leo inatufundisha kuwa mtu wa pekee aliye na haki ya kuhukumu ni Mungu. Ni Mungu
pekee anayeweza kutambua mema na mabaya; ni Mungu pekee anayeweza kuona maisha
ya mtu. Ni Mungu pekee anayeweza kuhukumu ikiwa mtu ni gugu au ngano. Badala ya
kuhukumu wengine, kila mtu ajibidiishe kung’oa magugu madogo madogo yaliyo
katika mioyo na nafsi yake mwenyewe. Injili ya leo inatualika tujue kuwa Mungu
anatutarajia sisi. Mungu anataka tuanglie mambo yanayoendelea katika maisha
yetu. Wacha tufanye kazi pamoja naye ili kuto “magugu” katika utu wetu. Ndipo tuanze
kuwasaidia tunaowadhania ni “waovu” kama Kristo alivyofanya. Je! Kwa nini
hakumtoa Yuda aliyemsaliti, au Petro, ambaye alimakan? Yesu aliona “magugu”
maishani mwao, lakini pia akaona ngano. Alikua kuwa kwa kuwatia moyo ngano
ingechipuka. Na mara nyingi ilifanya, “Hata mtu mwaminifu Zaidi akiiba kitu
maishani mwake, hii haimaanishi kuwa watu wote ni wezi.”
No comments:
Post a Comment