Dominika ya 3 ya Pasaka, Aprili 26, 2020, Mwaka A
Injili 24:13-35
Katika
Injili ya leo, tulisikia watu wawili walikuwa wakienda katika kijiji kiitwacho
Emausi. Watu wengine walisema kuwa walikuwa pia wanafunzi wa Yesu Kristo. Je!
Kwanini walikuwa wanaondoka Yerusalemu? Kwa sababu walikatishwa tamaa.
Waliamini kuwa Yesu ndiye Masihi wao, lakini alisulubiwa na kuuawa. Kwao,
Yerusalemu ikawa mahali pa uchungu, huzuni na tamaa. Walihuzunika na kusikitika.
Hakukuwa na sababu ya kubaki Yerusalemu. Kwa hivyo ilibidi wasafiri kwenda
kijiji cha Emausi kuepuka maumivu yao, huzuni na tamaa. Lakini Yesu aliandamana
nao. Na wakati aliumega mkate, walimtambua Yesu na alirudisha tumaini la maisha
yao. Walifurahi mara nyingine tena. Na walifanya nini? Walirudi Yerusalemu.
Sasa, Yerusalemu haikuwa mahali pa kifo lakini uzima, haikuwa mahali pa huzuni,
bali mahali pa furaha. Je! Tunaweza kujifunza nini kutoka kwa Injili ya leo?
Safari ya wanafunzi kwenda Emau inaanza na huzuni, na kukata tamaa. Lakini
inaisha kwa furaha na tumaini. Hadithi yao sasa ni hadithi iliyojawa na maisha
na tumaini.
Hadithi
ya Emmaus inatusaidia kuelewa kwamba hatutembei peke yetu. Yesu yuko pamoja
nasi. Maisha yetu ni safari na Yesu ndiye njia na tumeitwa kumfuata. Inaonekana
kuna wakati tunajihisi upweke na tuko peke yetu lakini Yesu yuko nasi wakati
wote na katika hali zote. Yesu hujifunua katika Ekaristi Takatifu wakati wa
kuvunja mkate ikiwa ni shara ya kuwaunganisha wakristo na jumuia zote katika
mwili wa kristo na Anawasiliana nasi na kuzungumza nasi katika Maandiko.
Hadithi ya wanafunzi hawa wawili ni hadithi yetu. Ningependa ukumbuke
nyakati ambazo ulipotezatumaini na kukata tamaa. Kumbuka nyakati ambazo maisha
yako yalikuwa yamejawa na huzuni na maumivu. Kumbuka nyakati ambazo tulitamani
kurejesha tumaini, Kumbuka, nyakati ambazo ulitaka kukatisha uhai wako, na
kumbuka nyakati ambazo maisha yetu hayakuwa na maana? Bwana wetu Yesu Kristo
hajawahi kutuacha. Katika nyakati zote hizo ngumu za maisha yetu, Yeye
hufuatana nasi kila wakati, na atarejesha ustawi wetu, Atarudisha shangwe na
furaha yetu katika maisha yetu. Tumtwishe fadhaa zetu, hofu na wasiwasi wetu
tumtwike yeye.
Siku moja, baba na mtoto
walikuwa wanavuka mto. Baba akamwambia, mwanangu, nishike mkono wangu ili
nisizame katika mto. Mwana akajibu, baba, nishike wewe mkono wangu, kwa sababu
mto ukiwa na kina kirefu naweza nikakuachia, lakini ikiwa utanikamata wewe
mkono wangu najua kuwa hautaniacha kamwe.
No comments:
Post a Comment