Dominika ya 2 ya Pasaka, Aprili 19, 2020, Mwaka A
Injili: Yn 20: 19-31
Injili
ya leo inatueleza ambacho Yesu Kristo alifanya baada ya kufufuka Kwake.
Wanafunzi wake walikuwa wamekusanyika katika chumba kidogo. Walikuwa bado
wakiogopa Wayahudi kwamba Wayahudi watawaua kwa kuwa walikuwa wafuasi wa Yesu
Kristo. Kwa ghafla bila kutegemea kabisa, Yesu aliwatokeza mbele yao.
aliwaonyesha mikono yake na pande zake zilizotobolewa na misumari. Aliwapa ujumbe wa amani na aliwaahidi kwamba
amani Yake haiwezi kuondolewa kutoka kwao. uwepo wa Yesu ilikuwa ishara ya
amani.
Wakati
Yesu alipowatokeza wanafunzi wake kwa mara ya kwanza, ni kumi tu waliokuwepo.
Tunaambiwa kuwa, kwa sababu fulani, mmoja wa wanafunzi, Tomaso, hakuwepo kwenye
hafla hii. Hatujui kwanini hakuwepo. Kilicho muhimu ni kukutana kwake na Yesu
Aliyefufuka. Alikataa kuamini kuwa Bwana amefufuliwa kutoka kwa wafu na
alikuwepo kati ya wafuasi wake. Alitaka kuona kwa macho yake mwenyewe na
alitaka kugusa mwili wake. Tomaso binafsi alitaka kukutana na Yesu ili kuamini
ufufuo wake. Je! Kwanini Tomasi hakuamini juu ya ufufuko wa Yesu Kristo?
Walipomwambia kwamba Yesu amefufuka na ameonekana kwao labda alishangaa na
akajiuliza basi kwanini bado mnajificha? Alihisi kama wangemwona Yesu kweli
wangekuwa wakipiga kelele kwa sauti ya juu wakiuambia ulimwengu kuwa Yesu yu
hai. Kwa kuwa wamejificha na walikuwa bado wanaogopa Wayahudi, hakuweza kuamini
amefufuka. Kwa kweli Tomaso alikuwa mtu wa imani. Katika maisha yake alifanya
hivyo tu. Alienda mbali sana India na akafa kwa imani yake.
Kama
tunavyojifunza katika Injili, Yesu alionekana wiki moja baadaye siku ya
Jumapili, na alikutana nao kwa mara nyingine akawatakia Amani. Kisha akamwita
Tomaso akamkemea kwa kutokuamini kwake, akamwamuru amshikeshike na kupapas
mikono yake ili aamini. Je! Alimgusa Yesu Kristo? Maandiko yanatuambia kuwa
macho ya Thomaso yalifunguliwa na kutamka kwa Imani. "Bwana wangu na Mungu
wangu!" Wakati huo, lazima Tomaso alistaajabu na kushangaa. Mwisho wa tukio
hili, Yesu alimpongoza Tomaso kwa imani yake kwake mara tu alipokutana naye.
Yesu aliwahimiza wanafunzi wake kuaminipasipo
kuona. Imani kwa kweli ni kukutana na Mungu kwa jicho la ndani la kiroho na
kumtegemea. Na kweli tangu sasa, ufuasi wa Yesu ni kumwamini pasipo kumwona,
lakini ni kutunza ushuhudo kuwa Yesu yu hai, kwamba yeye yuko pamoja nao katika
yote wanayofanya, kwamba yeye ndiye chanzo cha amani yao na furaha katika
majaribu yao yote na dhiki.
Je!
Tunaweza kujifunza nini katika kwa Injili ya leo? Kwanza, hofu ni kinyume cha
imani katika Mungu. kama wanafunzi tunaweza kuwa na woga mwingi. Hofu ya
kupoteza kazi, woga wa kupoteza utajiri wetu, woga wa kupoteza maisha, hofu ya
hatma yetu. Lakini sikukuu ya ufufuo inatuambia kwamba Yesu Kristo ametukomboa
katika woga wetu na wasiwasi. Tunachohitajika kufanya ni kumwamini kila wakati.
Kwa kumwamini Yesu Kristo tutashinda woga wetu. Kuogopa kitu chochote
hututenganisha na Mungu. Pili, ni vizuri kujiuliza kuhusu uwepo wa Mungu katika
maisha yetu. Tomaso alitafakari kufufuka kwa Yesu Kristo. Lakini bado alikuwa
tayari kujifunza zaidi juu ya Yesu Kristo. Hata alienda India kuhubiri neno la
Mungu. Ni vizuri kutafakari uwepo wa Mungu katika maisha yetu haswa tunapopitia
magumu katika maisha yetu. Lakini tunatakiwa kuwa tayari kama Tomaso ili
tufundishwe na Yesu Kristo. Tafakari
zetu juu ya uwepo wa Mungu unaweza hata kuimarisha imani yetu. Tunahitaji
kumruhusu Yesu Kristo aongoze maisha yetu. Tunahitaji kutoa maisha yetu kwa
Yesu Kristo na kwa mara nyingine tutahisi uwepo wa Mungu katika maisha yetu.
Matatizo na shida zetu katika maisha yetu ziko ili kutuimarisha, na kuimarisha
imani yetu kwa Yesu Kristo.
Mtu
mmoja alikuwa na shida nyingi maishani mwake. Kwa hivyo aliomba Mungu aingilie
kati katika maisha yake na atatue shida zote. Aliomba mchana na usiku na siku
moja akasikia sauti kutoka juu ikisema: "Nataka uende kusukuma jiwe hilo
kubwa.” Mtu huyo aliamka na akiwa na shauku. Alikimbia kutafuta lile jiwe na
kuanza kulisukuma. Alisukuma na kusukuma, lakini hakuambulia chochote.
Aliendelea kusukuma mwamba huo kwa siku
nzima. Siku iliyofuata alifanya vivyo hivyo, lakini jiwe halikuhama hata
kidogo. Kwa miezi mitatu mtu huyo aliendelea kusukuma
mwamba mkubwa. Mwishowe alichoka na akaacha kusukuma. Usiku huo aliota ndoto
nyingine, na akasikia sauti ikisema: "Kwa nini umeacha kusukuma
jiwe?" "Hakuna kilichobadilika katika maisha yangu, bado kuna shida
na jiwe bado liko pale pale," - akajibu mtu huyo. "Hakuna
kilichotokea? Jitazame mwenyewe! Umekuwa mtu imara na mwenye kujitambua
Zaidi. Umekuwa shupavu Zaidi. Wewe ni
mtu aliyebadilishwa sasa! Kusukuma kumekubadilisha! Hata hivyo, sikukuambia uliondoe
jiwe. Nilikuambia usukume tu. Wakati utakapofika, nitaliondoa mwenyewe! "Kama
unavyoona, wakati mwingine magumu katika maisha yako yapo ili kukufanya uwe
imara na kukubadilisha. Matatio hayapo ili uyaondoe wewe nao. Wakati ukifika, Mungu
wetu atatuokoa kutoka katika shida zetu.
No comments:
Post a Comment