Somo la Kwanza. Mdo.2:14a, 36-41
Somo la Pili. 1Pet. 2:20b-25
Injili. Yn. 10:1-10
Jumapili ya nne ya Pasaka inajulikana kama jumapili
ya Mchungaji Mwema, kama Yesu anavyo jiongelea mwenyewe kuwa ni “Mchungaji
mwema”. Yesu anatupa sura ya Mchungaji mwema anaye wafahamu kondoo wake:
anawaita, anawalisha na kuwaongoza. Ni kwasababu ya hili Kanisa limeipendekeza
kuwa siku ya kuombea miito duniani.
Yesu anaonesha wazi tofauti ya wachungaji. Tofauti
anayotoa ni juu ya mchungaji yule anaye wafahamu kondoo wake na kuwajali, na
wale wanaofuata tu mkumbo bila sadaka ya upendo. Yesu alitolea sadaka kamilifu
kama Mchungaji wa Kimungu. Alikuwa yupo tayari kutembea nasi katika njia zote,
sisi kondoo wake. Alikuwa yupo tayari kutoa sadaka ya kila kitu. Hakutaka
mateso, kuonewa, kukataliwa na mambo mengine yamuondoe kutoka katika lengo lake
la kuwajali na kuwatunza watu wake katika njia kamili. Inapaswa ituguse na
sisi, kutufariji na kutupatia sisi ujasiri na kutambua ni kwa jinsi ghani
upendo wake ulivyokuwa mkubwa kwetu.
Katika hali nyingine Yesu anaongea kuhusu mfano wa
mtu mwingine ambaye sio mchungaji mwema, ambaye anaona mbwa mwitu wakija na yeye
hukimbia. Tunapaswa kuona ndani ya mtu huyu, vishawishi vyote ambavyo vyaweza
kuja katika maisha yetu. Ni vigumu kubaki wakati wa nyakati ngumu. Ni vigumu
kuwa karibu na wale wenye shinda wanapo tuhitaji sisi. Ni vigumu kuwa waminifu
mpaka mwisho bila kuwa na aibu tunapo kutana na vishawishi vya hofu. Yesu
anatupa nguvu na msaada wa upendo kamili yeye akiwa kama Mchungaji wetu mwema,
lakini pia anatuhitaji nasi turudishe upendo huu huu kwake, kwa kuwapatia
wengine upendo huu huu mkamilifu. Pale ulipo shindwa na kupungukiwa tunamuomba
yeye akuchunge kama mchungaji ili nawe uweze kuwachunga wengine. Mkimbilie
mchungaji mwema na amini upendo wake kwako.
Leo, Kanisa zima linatukumbusha hitaji letu la
kuomba, kama Yesu mwenyewe alivyo waambia wanafunzi wake, hivyo kwamba
"mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake"
(Lk 10: 2). Tangu hapo awali Kanisa “ kwa asili yake ni umisionari" (Ad
Gentes, 2), wito wa Ukristo unazaliwa ndani ya watu kutokana na kazi ya
umisionari. Katika siku hizi kwanza
tunaombwa tuombee Kanisa liweze kupata wachungaji wema na waadilifu wa kufanya
kazi ya Kristo ya kueneza Injili, na kwamba Kanisa liweze kupata vijana wengi
wanoitwa kwenye wito wa upadre na utawa ikiwa ni pamoja na watoto wetu wenyewe.
No comments:
Post a Comment