Tafakari ya Alhamisi Kuu
Injili: Yn. 13:13:1-15
Wakati
wa Yesu Kristo, barabara za Palestina zilikuwa chafu na zenye matope. Wakati wa
kiangazi, zilikuwa na vumbi sana na wakati wa mvua zilikuwa na matope. Hakukuwa
na mabasi, baiskeli au pikipiki, watu daima walitembea umbali mrefu. Watu
hawakuvaa viatu, walivaa kandambili tu. Kwa hivyo miguu yao ilikuwa michafu
kila wakati. Kwa hivyo kila walipoingia ndani ya nyumba, ilibidi waoshe miguu
yao. Kawaida, kazi ya kuosha miguu ilifanywa na watumwa, watoto, na wanawake,
wale ambao hawakuweshimika katika jamii. Inadhihirisha ukweli wa Jumuiya ya
Yesu. Mabwana hawakuosha miguu ya wageni. Wale ambao wenye mamlaka, utajiri,
akili, uzuri na vyeo huoshwa. Wale ambao wasio na nafasi ndio waliosha wenzao.
Lakini katika Injili ya leo Yesu kama bwana kama mesia aosha miguu ya wanafunzi
wake. Ulimwengu wetu sio tofauti sana na wa Petro.
Lakini
usiku huu ni tofauti, uoshaji huu wa miguu ni tofauti. Kwa mara nyingine Yesu
anavunja sheria na utaratibu wa kijamii. Wakati wa chakula cha jioni Yesu
anainuka kutoka kwenye meza, anaondoa vazi lake, anafunga kitambaa, anamwaga
maji ndani ya bonde, na anaanza kunawisha miguu ya wanafunzi. Wanafunzi wote
wanashangaa, haswa Petro hakuelewa kile kinachoendelea. Ufahamu wa Petro
unabadilishwa na yeye hapendi. Fikiria juu ya mara ya mwisho ulimwengu wako
kubadilika au kutishia kubadilika. Kama mabadiliko hayo yana faida nyingi kwetu
tunapinga, tunakasirika, na tunapambana. Tunalalamika juu yake na kejeli kwa
kuyashambulia kwa rafiki zetu tuanowaamini.
"Hautaniosha
miguu yangu kamwe," Petro anajibu. "Ninashikilia kile ninachojua.
Sitaki univurugie ulimwengu wangu na jinsi nilivyozoea. " Petro hataki
kubadilisha mila. Wakati mwingine hata sisi tuko kama huyu; labda hatutaki
mabadiliko katika familia zetu na katika Kanisa letu. Tunataka kushikamana na
yale ambayo tumezoea. Kama kuhani ikiwa nitaleta mabadiliko madogo Kanisani,
watu watauliza, kwanini unataka kutuvuruga, tumezoea njia za zamani. Katika
sehemu zetu za kazi, ikiwa mtu ataleta mabadiliko, tunasema ni kwanini
unatuvuruga wakati tulikuwa sawa na tulichokuwa tunafanya, kwanini unataka
kututesa? Kwa vitu vyovyote vipya tunasema kila wakati "Hatujawahi kuenenda
namna hii na hatuna nia ya hayo mabadiliko. Usitusumbue na kutuvuruga.
Peter
hakutaka usumbufu, Petro hakutaka mabadiliko, Patro alijisikia vizuri na mila
za zamani. Ndio maana hataki Yesu aoshe miguu yake kwa sababu ilikuwa kawaida kwamba
watumwa waoshe miguu ya Bwana. Baada ya kuosha miguu ya wanafunzi wake, anawaambia
"lazima muoshe miguu ya kila mtu." Kwa maana nimewafanya vielelezo
vya kwamba ninyi pia mnapaswa kufanya kama vile nilivyofanya kwenu. Yesu ametuonesha
mfano wa upendo mbele yetu. Hakuna miguu iliyotengwa na upendo. Hakuna miguu
isiyostahili kuoshwa. Hata miguu ya akina Yuda ilioshwa. Kuna miguu mingi. Miguu
ya Vijana, wazee, waliochoka, waliopotea, waliofadhaika, wenye hasira na
walioumizwa.
Kuna
kila aina ya miguu. Miguu ambayo imepitia katika vitu vichafu vya maisha. Miguu
ambayo imepita katika sehemu zilizozuiliwa. Miguu ambayo imesimama kwenye ardhi
takatifu. Miguu ambayo imebeba ujumbe wa habari njema. Hiyo ndiyo miguu
aliyoosha Yesu. Ni miguu ya ulimwengu. Ni hii ambayo Yesu anatuamuru kuosha. Hi
yenyewe kabisa haitofautinai na miguu yetu. Sisi pia tumepitia vitu vichafu vya
maisha. Miguu yetu pia imepita katika maeneo yaliyozuuliwa. Miguu yetu
imesimama kwenye ardhi takatifu. Miguu yetu imebeba ujumbe wa habari njema. Kwa
hivyo Yesu anaposema kufuata mfano wangu, haimaanishi kwamba tunapaswa kurudia
ibada hii kila Alhamisi Takatifu. Hakuwa akituambia tuoshe watu 12 katika
parokia zetu. Alitupatia ufahamu wa utume wake na maisha yake, na kwa hivyo,
alipendekeza kwa wanafunzi wake.
Kweli,
aliwakabidhi utume huu wa huduma ya upendo, ambayo ni sawa na yetu leo. Yeye
anatupa utume uleule sio tu kwa mapadre na masista bali sisi wote
tuliokusanyika hapa. Yesu alimpokea kila mtu, wagonjwa, makahaba, wazuri na wabaya
na Alishiriki upendo wake kwa kila mtu kwa usawa hata msalabani. Je! Ni nini wajibu
yetu kwa mwaliko wake wa kupenda wote? Alhamisi Takatifu sio juu ya kuosha
miguu ya watu 12. Ni juu ya kushika na kufuata na hatua za Yesu kwa jinsi tunavyoshirikiana
na wengine. Kwa kuosha miguu Yesu anatuonehsa mfano katika maisha yetu, mfano
wa maisha yenye upendo na unyenyekevu. Wote tunaalikwa kufuata mfano huu wa
upendo na huduma. Na kwa hivyo, ninagundua kuwa kunawa miguu sio tukio la kila
Alhamisi Takatifu lakini ni njia ya maisha ya kila siku. Omba, kwa hivyo,
kwamba sherehe hii ya Alhamisi Tukufu inaweza kutia msukumo wa kupita zaidi ya
ibada nzuri!